Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

SIKU 8 YA 31

Lawi ambaye kwa jina jingine ni Mathayo (Mt 9:9) aliokoka. Furaha yake ya kumjua Yesu alitaka kuwashirikisha watu wa nyumbani mwake pamoja na rafiki zake. Naamini hata Tanzania mtu akiokoka atafanya hivyo. Kama wewe ni baba wa nyumba ni nani atakayekuzuia usifanye karamu? Kwa vyo vyote mtu akimpokea Yesu ni muhimu mara moja ashuhudie hali yake mpya mbele ya watu ili asirudi nyuma na ili Mungu apewe sifa. Kumbuka ilivyoandikwa katika Rum 10:9-11: Ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika. Katika m.35 Yesu anasema, Siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi, ndipo watakapofunga siku zile: Hii ni hali tuliyo nayo sasa hadi arudipo Yesu. Fikiria Mt 6:16-18 uone Yesu anavyotukumbusha akisema, Mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma k...

More

http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha