Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

SIKU 10 YA 31

Wanafunzi wa Yesu walikuwa wengi (m.17). Kati yao aliwachagua Mitume 12 bila kuangalia kabila lao. Idadi hii ni sawa na idadi ya makabila ya Waisraeli. Waisraeli walikuwa ni watu wa Mungu. Kwa kutumia idadi hii hii ya 12 Yesu alitaka kuonyesha kwamba sasa huweka msingi mpya kwa watu wa Mungu. Sasa kuhesabiwa kuwa mtu wa Mungu hakutategemea tena kabila la mtu bali itategemea uhusiano wake na Yesu Kristo, Mwana wa Mungu! Taifa hili jipya alilotengeneza Yesu aliliita kanisa! Mistari ifuatayo inathibitisha hiyo: Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda (Mt 16:18). Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni (Efe 2:19-20).

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

http://www.somabiblia.or.tz