Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

SIKU 12 YA 31

Yesu aliwapa wanafunzi wake maneno ya faraja, maagizo ya kufuata na maneno kwa ajili ya kujichunguza. Kila mtu ajihoji kama amejenga kwenye msingi ulio imara au ulio mbovu. Yesu anauliza, Kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo? Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake. Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri. Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba ile yakawa makubwa (m.46-49). Katika Zab 139,23-24 kuna neno zuri la kuomba kama itikio la maneno hayo ya Yesu: Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu; Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele. Tafakari piam.37: Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa. Alama ya Mkristo wa kweli siyo roho ya kuwahukumu wengine bali ni roho ya upendo. Ni roho inayojifahamu kwamba mimi ni mwenye dhambi ninayehitaji kila siku msamaha wa Mungu. Mfano wa haya ni jinsi Bwana Yesu alivyotufundisha kuomba: Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu (Mt.6:12; ukiwa na nafasi soma pia Lk 18:9-14 na Yn 8:1-11).

siku 11siku 13

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma k...

More

http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha