Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

SIKU 11 YA 31

Umati wa watu walikuja kwa Yesu. Yesu alitumia nafasi hii nzuri akatoa hotuba juu ya Ufalme wa Mungu. Lakini angalia, aliwalenga kipekee wanafunzi wake yaani waliokuwa wamepata tayari uraia wa ufalme huo kwa kuzaliwa kwa Roho. Maana bila Roho wa Mungu mtu hawezi kufuata wala kuelewa maagizo ya Yesu katika hotuba hii. Luka ameandika hotuba yake kwa ufupi zaidi kuliko Mathayo (Mt 5:1-7:29). Kwa wenye taabu Yesu hutoa faraja kubwa akisema, Heri ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashiba. Heri ninyi mliao sasa, kwa sababu mtacheka. Heri ninyi watu watakapowachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu. Furahiwani siku ile na kuruka-ruka, kwa kuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana, baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo (m.21-23). Lakini kwa wenye raha Yesu hutoa onyo kali:Ole wenu ninyi mlio na mali, kwa kuwa faraja yenu mmekwisha kuipata. Ole wenu ninyi ambao mmeshiba sasa, kwa kuwa mtaona njaa. Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, kwa kuwa mtaomboleza na kulia. Ole wenu ninyi watu wote watakapowasifu, kwa kuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo (m.24-26). Je, wewe u katika kundi gani? U heri?

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma k...

More

http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha