Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

SIKU 7 YA 31

Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi (m.24). Kwa neno hili Yesu alisisitiza mambo mawili. 1. Yeye ni Mwana wa Mungu, maana ni Mungu peke yake awezaye kusamehe dhambi. Hili ni hoja ya Yesu anapowajibu waandishi na Mafarisayo katika m.21: N'nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake? 2. Alifanya mwujiza wa kumponya huyo mgonjwa ili kuthibitisha kwamba anayo kweli amri ya kusamehe dhambi. Kwa hiyo dhambi za huyo mtu zilisamehewa kweli. Kuondoa dhambi ni shabaha kuu ya kazi ya Yesu. Maana uzima wa milele ni muhimu kuliko uzima wa maisha haya. Ndiyo maana yake, Yesu akiuliza, Itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake? Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu (Mk 8:36-38). Kumbuka pia kusudi kuu la Yesu kuzaliwa: Ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao (Mt 1:21).

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma k...

More

http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha