Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022

SIKU 31 YA 31

Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa (m.21). Neno ”watu wote” linatupa picha ya ukubwa wa huo uamsho. Kwa nini Yesu alibatizwa? Je, alihitaji kuondolewa dhambi? Hapana. Lakini wote waliotangulia kubatizwa waliweza kutangaziwa msamaha wa dhambi kwa sababu moja tu, yaani, Yesu! Yeye ndiye Mwana-kondoo wa Mungu. Alipobatizwa alikubali kuchukua mzigo wa dhambi za wanadamu wote na kujitoa kama sadaka msalabani ili kutupatanisha na Mungu! Mistari ifuatayo inasema zaidi juu ya jambo hili: Yohana alipomwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu (Yn 1:29)! Na Yohana mwingine aliandika, Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote. … Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu (1 Yoh 2:1-2; 4:10).

siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

Mipangilio yanayo husiana

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha