Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022

SIKU 1 YA 31

Zekaria ni miongoni mwa manabii wa taifa la Israeli. Ujumbe wake ni wa kihistoria (m.1) na wa kweli: Mungu alitenda alivyosema. Kwa hiyo anawahoji waliomsikiliza Zekaria: Maneno yangu, na amri zangu nilizowaagiza hao manabii, watumishi wangu, je! Hazikuwapata baba zenu? Nao wakageuka na kusema, Vile vile kama Bwana wa majeshi alivyoazimia kututenda, sawasawa na njia zetu, na sawasawa na matendo yetu (m.6). Sasa anawaita watu watubu vivyo hivyo. Waungame uovu wao kabla hawajaadhibiwa. Nirudieni mimi, asema BWANA wa majeshi, nami nitawarudia ninyi … Msiwe ninyi kama baba zenu (m.3-4). Tukubali historia itufundishe. Neno la Mungu lipo, likitenda kazi. Toba ya kweli ni kurudi kwa Bwana. Pasipo kurudi kuna majuto. Tunaitwa kulishika kwa kuliamini, kulitii na kuliishi.

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha