Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022

SIKU 27 YA 31

Wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu [Ana] akawatolea habari zake [Yesu] (m.38b). Yerusalemu kulikuwepo na waumini waliokuwa wakitazamia kwa hamu sana Mungu atimize ahadi zake za kumtuma Mkombozi. Kati yao ni hao wazee Simeoni na Ana (m.25-26). Kuhusu Simeoni imeandikwa kwamba alimshukuru Mungu kwa kusema, Macho yangu yameuona wokovu wako, uliouweka tayari machoni pa watu wote; nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, na kuwa utukufu wa watu wako Israeli. Hata siku hizi katika nchi ya Tanzania wapo waumini wanaotarajia ukombozi kutokana na ahadi za Mungu, yaani, kurudi kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Wako mijini na pia vijijini. Ebr 9:27-28 inaeleza habari za hao wamtazamiao kwa wokovu. Je, u mmojawao?

siku 26siku 28

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha