Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022

SIKU 23 YA 31

Zakaria alipomsifu Mungu alitabiri pia juu ya watoto hao wawili: Yohana na Yesu. M.68-75 na 78-79 inamhusu Yesu. Jina ”Yesu” maana yake ni ”Bwana anaokoa”. Kuja kwake ni kuja kwa wokovu hapa duniani. Ni Mungu kutimiza mpango wake aliokuwa nao tangu awali ambao ulitabiriwa na manabii. Ametusimamishia pembe ya wokovu ... Kama alivyosema tangu mwanzo kwa kinywa cha manabii wake watakatifu (m.69-70). Wokovu hasa unahusu kuondolewa dhambi(Mt 1:21, Yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao). Kazi ya Yohana italenga jambo lilo hilo, yaani, kuwajulishawatu wake wokovu katika kusamehewa dhambi zao (m.77).

siku 22siku 24

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha