Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

SIKU 10 YA 31

Hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu. Kwa hiyo mtu mwenye tabia ya kidunia, hampokei Kristo. Hata akielewa maneno, anayadharau. Anaona hakuna faida, hajui maana yake kwake. Habari njema ya Kristo inaendelea kuwa siri, maana kutambua siri ya Kristo kunawezeshwa na Roho Mtakatifu tu. Yeye ndiye chombo cha kukuwezesha na kukuelimisha wewe juu ya kile Mungu akitakacho kwako. Je, u tayari kupokea baraka hiyo? Atawapa Roho Mtakatifu wale wanaomwomba (Lk 11:13, Ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?).

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kuji...

More

Tungependa kushukuru kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha