SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20Mfano

Katika mlango huu tunajulishwa amri kumi za Mungu. Amri hizi zinagawanyika katika mafungu makuu mawili. Amri tatu za kwanza zinahusu uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu. Ni uhusiano baina ya Mwumbaji na kiumbe wake. Kwa vyovyote vile, ukizishika vema amri za Mungu unapata pia mwongozo wa jinsi ya kuhusiana na wanadamu wenzako. Yesu Kristo anakamilisha amri hizi kwa kusema kuwa amri kuu kuliko zote ni upendo, yaani, kumpenda Mungu na jirani zetu. Zingatia maneno yake katika Mk 12:29-31: Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Kutoka, Zaburi na Isaya. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Anza mwaka wa 2020 kwa kujifunza Neno la Mungu kupitia mpango huu.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz
Mipangilio yanayo husiana

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Upendo Wa Bure

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?

Soma Biblia Kila Siku 11/2020

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021
