SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20Mfano

Kwa nini watu waliambiwa hawawezi kumwona Mungu? Ni kwa sababu Mungu ni mtakatifu, na wanadamu ni wenye dhambi. Wanadamu walipoteza utukufu wa kuonana na kukaa karibu na Mungu pale walipovunja amri ya Mungu katika bustani ya Edeni. Kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa [mtu]katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa. Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima(Mwa 3:23-24). Kuja kwa Yesu kumeondoa wingu lililokuwa linazuia wanadamu wasiuone uso wa Mungu Mtakatifu. Damu ya Yesu ndiyo inayoleta utakaso wa kudumu. Bila kutakaswa kwa damu hiyo hakuna uwezekano wa kukutana na Mungu. Damu ya Yesu inatosha kutupeleka katika wokovu wa kweli.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Kutoka, Zaburi na Isaya. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Anza mwaka wa 2020 kwa kujifunza Neno la Mungu kupitia mpango huu.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz
Mipangilio yanayo husiana

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Upendo Wa Bure

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?

Soma Biblia Kila Siku 11/2020

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021
