SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20Mfano

Kukutana na Mungu aliye mtakatifu kunahitaji maandalizi. Utaratibu wa maandalizi haya unatolewa na Mungu mwenyewe: Bwana akamwambia Musa, Njoo huku juu kwangu mlimani, uwe huku; nami nitakupa mbao za mawe na ile sheria na hiyo amri niliyoiandika ili uwafundishe (m.12). Musa anaamriwa na Mungu awaandae wana wa Israeli ili wakutane naye. Mungu ambaye ni mtakatifu, ndiye anayechukua jukumu la kuwaandaa watu wake, ambao ni wakosaji, ili wapate uwezo wa kukutana naye. Je, unajua Mungu amefanya nini ili kukutana na wewe na mimi? Katika Ebr 1:1 imeandikwa: Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana. Na Mwana huyu, yaani Yesu, anasema, Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha(Mt 11:28). Ni upendo, huruma na wema wa Mungu kwamba Yeye aliye Mtakatifu anatualika sisi wenye dhambi kwenda kwake!
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Kutoka, Zaburi na Isaya. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Anza mwaka wa 2020 kwa kujifunza Neno la Mungu kupitia mpango huu.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz
Mipangilio yanayo husiana

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Upendo Wa Bure

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?

Soma Biblia Kila Siku 11/2020

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021
