YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 04/2025Sample

Soma Biblia Kila Siku 04/2025

DAY 13 OF 30

Jumapili ya leo tunakumbuka siku ya mitende. Hii siku imepewa jina lake kwa sababu wakazi wa Yerusalemu walimpokea Yesu akiwa amepanda mwana-punda kwa mashangilio ya matawi ya mitende kama ishara ya kumpa heshima.Watu wengi wakatandaza mavazi yao njiani, na wengine matawi waliyoyakata mashambani(Mk 11:8). Ingawa watu hawa walionyesha heshima kwa Yesu, siku chache baadaye walipiga kelele kuwa asulubishwe. Kwa nje walionyesha wanampenda, lakini mioyoni mwao walikuwa kinyume naye. Usiwe mnafiki. Ukimpenda Yesu, maanisha hivyo kwa moyo wako wa ndani kwa kweli kabisa.

Scripture

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 04/2025

Soma Biblia Kila Siku 04/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Aprili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Walawi, Luka na 2 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu

More