YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 03/2025Sample

Soma Biblia Kila Siku 03/2025

DAY 28 OF 31

Wakati Nahashi, mfalme wa Amoni alipokufa, Daudi alipeleka salamu za rambirambi kwa Hanuni, mwanawe. Lengo la Daudi lilikuwa kuonesha kwamba alitaka kuendeleza mahusiano mazuri kati ya falme hizo mbili, lakini ujumbe wake ulitafsiriwa vibaya na wakuu wa Waamoni. Walifikiri ni wapelelezi. Kwa jinsi walivyowatendea vibaya wajumbe wa Daudi walichochea vita. Lakini hata Waamoni walipowanunua Washami wawasaidie, walishindwa. Yoabu alimwambia Abishai, nduguye:Uwe hodari, tukajitie moyo mkuu kwa ajili ya watu wetu, na kwa ajili ya miji ya Mungu wetu; naye Bwana afanye yaliyo mema machoni pake(m.13). Zingatia neno hili lina maana gani kwako.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 03/2025

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu

More