Soma Biblia Kila Siku 03/2025Sample

Shetani anamchochea Daudi kuwahesabu Israeli. Yoabu anachaguliwa kuwa msimamizi wa zoezi hili. Anatoa onyo, ila Daudi hataki kumsikiliza. Uamuzi huu unaonesha Daudi kutomtegemea Mungu. Kwa hiyo Mungu anamtuma mwonaji Gadi kumwambia Daudi kosa lake; ndipo Daudi anakiri kosa. Ndipo Daudi anapewa kuchagua kati ya aina tatu za adhabu. Uamuzi wake tunausoma katika m.13:Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na nianguke katika mkono wa Bwana; kwa kuwa rehema zake ni nyingi sana; wala nisianguke katika mkono wa wanadamu. Uamuzi huu unakufundisha nini? Kama Daudi, tuwe tayari kujikabidhi mikononi mwa Mungu kwa kukiri makosa yetu mbele zake.Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote(1 Yoh 1:8-9).
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Related Plans

The Bible in a Month

Sharing Your Faith in the Workplace

Two-Year Chronological Bible Reading Plan (First Year-January)

Simon Peter's Journey: 'Grace in Failure' (Part 1)

You Say You Believe, but Do You Obey?

The Holy Spirit: God Among Us

When You Feel Like Roommates: 4 Day Plan to Help You Love (And Like) Your Spouse for Life

Everyday Prayers for Christmas

Gospel-Based Conversations to Have With Your Preteen
