YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 03/2025Sample

Soma Biblia Kila Siku 03/2025

DAY 2 OF 31

Si halali kwako kuwa na mke wa nduguyo(m.18). Kwa maneno haya Yohana Mbatizaji alikuwa amekemea dhambi ya Mfalme Herode. Ilikuwa ni hatari kubwa, lakini Yohana alimwogopaMungukuliko wanadamu. Na kweli, Mfalme Herode alikasirika, akamfunga Yohana gerezani. Mwisho Yohana akauawa, ila Herode mwenyewe hakupenda iwe hivyo,maana Herode alimwogopa Yohana; akimjua kuwa ni mtu wa haki, mtakatifu(m.20).Fundisho: Sifa nzuri ya mtumishi wa Bwana ina nguvu kubwa katika jamii! Yesu amelifafanua namna hii:Nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni(Mt 5:16).

Scripture