Soma Biblia Kila Siku 08/2024Sample

Gedalia alifanywa kuwa liwali wa watu waliobaki Yuda. Kule Mispa, jirani na Yerusalemu, alikutana na wakuu wa Yuda waliosalia nchini baada ya Wababeli kuteka Yerusalemu. Aliwatia moyo akiwashauri wakubali utawala wa Kibabeli,akawaapia wao na watu wao, akawaambia, Msiogope kwa ajili ya watumishi wa Wakaldayo; kaeni katika nchi; mkamtumikie mfalme wa Babeli; itakuwa vyema kwenu(m.24).Katika Yer 40:6 tunasoma kwamba Gedalia alifanya hivyo kwa msaada wa nabii Yeremia:Yeremia akaenda kwa Gedalia, mwana wa Ahikamu, huko Mizpa, akakaa pamoja naye kati ya watu wale waliosalia katika nchi.Pia Yeremia mwenyewe aliwatia moyo kwa maneno kama haya,Msimwogope mfalme wa Babeli, mnayemwogopa; msimwogope, asema Bwana; maana mimi ni pamoja nanyi, niwaokoe, na kuwaponya na mkono wake. …lakini … ikiwa mwakaza nyuso zenu kuingia Misri, na kwenda kukaa huko; basi, itakuwa, upanga mnaouogopa utawapata huko, katika nchi ya Misri, nayo njaa mnayoiogopa itawafuatia mbio huko Misri, nanyi mtakufa huko(Yer 42:11-16).Lakini walikataa, wakaja kumwua Gedalia baada ya miezi miwili hivi (muda huu mfupi unaonekana tukilinganisha m.8 na 25:Mwezi wa tano, … amiri wa askari walinzi, mtumishi wa mfalme wa Babeli, akaingia Yerusalemu. … Lakini ikawa katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania, mwana wa Elishama, mmoja wa wazao wa kifalme, na watu kumi pamoja naye, wakamwendea Gedalia, wakampiga hata akafa). Kisha hao waliomwua mfalme wakakimbilia Misri. Inaeleweka kwa nini watu hao hawakutaka kumtumikia mfalme mgeni, lakini Mungu akisema, ni upumbavu kutotii.
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Related Plans

You Say You Believe, but Do You Obey?

Everyday Prayers for Christmas

The Bible in a Month

Never Alone

Sharing Your Faith in the Workplace

Simon Peter's Journey: 'Grace in Failure' (Part 1)

The Holy Spirit: God Among Us

Two-Year Chronological Bible Reading Plan (First Year-January)

Gospel-Based Conversations to Have With Your Preteen
