YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Sample

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023

DAY 25 OF 31

Hatuelewi kamili habari za siku ya Bwana. Somo lasema ni siku ya giza yenye kilio. Lakini angalia ni ujumbe kwa watu gani.Ninyi mnamkanyagamaskini, na kumtoza ngano...Ninyi mnaowaonea wenye haki, mnaopokea rushwa, na kuwageuza wahitaji langoni wasipate haki yao. Ndivyo Mungu anavyowatambulisha katika 5:10-12. Na huo udhalimu na ukatili wao wanauchanganya na ibada zao wakiamini hizo zitawaletea baraka tele. Lakini Mungu anasema katika m.21-22,Mimi nazichukia sikukuu zenu, nazidharau, nami sitapendezwa na makutano yenu ya dini. Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu ... sitazikubali.Kwaosiku ya Bwana ni mwanzo wa mateso yasiyokoma (ling. Mt 13:41-42,Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi, na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno). Kwa sababu gani? Kwa sababu siku ya Bwana itateremshahakikama maji makuu(m.24). Njia pekee ya kuepuka hukumu siku ya Bwana na kuwa na amani, sasa na milele, ni kutafuta leo kupatana na Bwana.

Scripture

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.

More