YouVersion Logo
Search Icon

Kuomba Kulingana Na Majina Yake Yesu: Nyota Ya AsubuhiSample

Kuomba Kulingana Na Majina Yake Yesu: Nyota Ya Asubuhi

DAY 4 OF 4

Nyota ya Asubuhi: Sala la Kusihi

“Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo haya kwa ajili ya makanisa. Mimi ndiye mzizi na mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.” Ufunuo 22:16

Yesu, nataka wengine walijue jina lako hili na wao wapate baraka za kuishi kulingana na mapenzi yako na njia zako.

Nipe busara ya jinsi ya kushiriki jina hili na wale walio karibu nami. Nionyeshe njia za kuwatia wengine moyo wa kukutafuta wewe na majina yako kikamilifu zaidi ili wakue katika uhusiano wao na wewe.

Niweke kwenye njia unayoiongoza wewe, nyota ya asubuhi, ili kwamba nisipotee njia yangu. Kwa unyenyekevu na shukrani zote, nakufuata wewe, nikijua kwamba kila hatua niliyopiga ili kunifikisha hapa nilipo leo ilichukuliwa tu kwa sababu wewe uliiangaza njia.

Naomba haya kwa jina lako. Amina.

Tunatumai kuwa mpango huu umekuhimiza. Ili ujue zaid kuhusu huduma ya Tony Evans, bofya hapa.