Kuomba Kulingana Na Majina Yake Yesu: Nyota Ya AsubuhiSample

Nyota ya Asubuhi: Sala ya Shukrani
“Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo haya kwa ajili ya makanisa. Mimi ndiye mzizi na mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.” Ufunuo 22:16
Yesu, asante kwa kuwa wewe ni taa inayoangaza mahali penye giza. Asante kwa kuwa sijaachwa nitembee kwa njia zangu mwenyewe na kutolewa kwa hofu mahali pa giza.
Unatoa nuru ili nifuate. Unainua kichwa changu ninapoogopa kutazama juu. Wewe ndiye nyota ya asubuhi ambaye unanitia moyo kuendelea kutembea nikijua kwamba siku mpya iko kwenye upeo wa macho. Kama vile 2 Petro 1:19 inavyosema,
“Basi tunalo neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo mwafanya vema kulisikiliza, kama taa inayoangaza mahali penye giza, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.”
Asante kwa neno la kinabii lililohakikishwa ndani yako, nyota ya asubuhi ikizuka moyoni mwangu.
Naomba haya kwa jina lako. Amina.
About this Plan

Dk. Tony Evans anatoa maombi ya jina la Yesu, nyota ya asubuhi. Sala ya kuabudu, maungamo, shukrani na dua kumhusu Nyota ya asubuhi, Yule anayeangazia njia yetu.
More
Related Plans

Simon Peter's Journey: 'Grace in Failure' (Part 1)

Biblical Wisdom for Making Life’s Decisions

When You Feel Like Roommates: 4 Day Plan to Help You Love (And Like) Your Spouse for Life

Never Alone

Two-Year Chronological Bible Reading Plan (First Year-January)

Gospel-Based Conversations to Have With Your Preteen

Sharing Your Faith in the Workplace

Everyday Prayers for Christmas

The Holy Spirit: God Among Us
