YouVersion Logo
Search Icon

Kuomba Kulingana Na Majina Yake Yesu: Nyota Ya AsubuhiSample

Kuomba Kulingana Na Majina Yake Yesu: Nyota Ya Asubuhi

DAY 2 OF 4

Nyota ya Asubuhi: Maombi ya Maungamo

“Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo haya kwa ajili ya makanisa. Mimi ndiye mzizi na mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.” Ufunuo 22:16

Yesu, mimi nashangaa jinsi maisha yangu yangekuwa tofauti ikiwa kama kwa kweli ningekuweka wewe uwe kama nyota ya asubuhi ya moyo na akili yangu. Jinsi gani maamuzi yangu yangekuwa ya hekima kiasi gani kama ningetegemea uongozi wako badala ya uongozi wangu.

Je, utanivumilia na utanipa neema kubwa zaidi ninapoiacha njia ya hekima yangu? Je, utaniongoza kwa upole kuelekea nuru yako ili niweze kuwa na dira ya huruma, wema na upendo katika maisha yangu?

Wewe ndiye kiongozi, Ee nyota angavu ya asubuhi. Wewe ndiye tumaini la wito wangu. Nisaidie ninaposhindwa na kupungukiwa kwa kukosa kutubu na kurudi Kwako, Yesu, nyota yangu ya asubuhi.

Haya nayaomba kwa jina lako. Amina.