YouVersion Logo
Search Icon

Kuomba Kulingana Na Majina Yake Yesu: Nyota Ya AsubuhiSample

Kuomba Kulingana Na Majina Yake Yesu: Nyota Ya Asubuhi

DAY 1 OF 4

Nyota ya Asubuhi: Maombi ya Kuabudu

“Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo haya kwa ajili ya makanisa. Mimi ndiye mzizi na mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.” Ufunuo 22:16

Yesu, ninakuabudu na ninalisifu jina lako, ee nyota angavu ya asubuhi.

Wewe ni mzizi na uzao wa Daudi. Umewatuma malaika wako kushuhudia nguvu na uwezo wako. Na tuwe na masikio ya kusikia na kupokea jina hili lako.

Katika jina hili, tunagundua nuru yako. Tunagundua uwepo wa mwongozo unaotoa. Tunafunua nuru ya hekima yako na mwelekeo utokao kwenye Neno lako. Ninakuheshimu kwa hekima, kweli na mwongozo wako ambao ninautegemea kila wakati wa siku yangu.

Ninakuabudu kwa jinsi unavyotafuta kutujulisha kila mmoja wetu utimilifu wa jina hili kuu.

Naomba haya kwa jina lako, Amina.