YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Sample

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

DAY 10 OF 31

Mungu akambariki Isaka! Baraka hizi zilionekana kwa njia mbalimbali: 1. Isaka alipopanda mbegu akapata mazao mengi (m.12, akapata mwaka ule vipimo mia kwa kimoja, Bwana akambariki). 2. Alikuwa na mifugo mingi na watumwa wengi (m.14). 3. Akawa mwenye nguvu sana kiasi cha Wafilisti kumwogopa (m.16, Abimeleki akamwambia Isaka, Utoke kwetu, maana wewe una nguvu sana kuliko sisi). 4. Kila alipochimba kisima akapata maji (m.19, Watumwa wa Isaka wakachimba katika lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika; pia m.32). 5. Akapata kukaa kwa amani na majirani zake (m.26-31, Wakasema, … hatukukutendea ila mema, tukakuacha uende zako kwa amani). Isaka alipata ukuu wake kutokana na baraka za Mungu tu! Hakuwa na tabia ya kuiba wala kupigana vita (m.16-17, 19-22; zingatia zaidi maneno haya, Isaka akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa Bwana ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi)! Ni mtu wa imani na amani!

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More