YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 07/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

DAY 7 OF 31

Mfalme Herode anayezungumziwa katika somo la leo alikuwa ni mwana wa Herode Mkubwa ambaye alikuwa mfalme wa Uyahudi wakati Yesu alipozaliwa. Alikuwa ni mfalme wa Galilaya na alitawala miaka 43. Lakini alikuwa na udhaifu wake. Udhaifu wake ni wanawake. Alikanyaga haki ya Mungu alipomwoa Herodia, mke wa ndugu yake. Na alikanyaga haki alipotimiza maombi ya Herodia ya kupata kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye kombe. Herodia alitaka hivyo kwa sababu Yohana alikuwa amelikemea tendo la mfalme la kumwoa yeye.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

Soma Biblia Kila Siku 07/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More