YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 07/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

DAY 12 OF 31

Huduma ya Yesu kuwaponya wagonjwa na kuwashibisha wenye njaa inaonyesha kwamba anampenda mwanadamu alivyo, haipendi tu roho ya mwanadamu bali na mwili pia. Wokovu wake si kwa ajili ya roho tu bali kwa ajili ya mwili pia. Kwa hiyo twakiri katika ukiri wa imani ya mitume kwamba "tunaamini ufufuo wa mwili"! Maana mwanadamu bila mwili si mwanadamu mkamilifu. Ufalme wa Mungu utakapokuja katika utukufu tutaishi humo tukiwa tumepata miili mipya isiyo na dhambi, miili ya utukufu. Maumivu na kifo havipo tena.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

Soma Biblia Kila Siku 07/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More