YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 07/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

DAY 1 OF 31

Kuna umoja mkubwa kati ya Yesu na wafuasi wake. Nguvu ya umoja huu Yesu anailinganisha na umoja wa kiukoo. Kwa hiyo kukubali kumwamini Yesu Kristo na kuwa mfuasi wake ni kukubali kuingia katika familia mpya, familia ya Yesu Kristo. Katika familia hii Mungu ni Baba yako na Yesu ni ndugu yako. Na Wakristo wengine ni ndugu zako, na baadhi yao ni kama baba na mama kwako. Msingi wa umoja huu ni kufanya mapenzi ya Baba wa Yesu ambayo ya kwanza ni kumwamini Mwana wake, Yesu Kristo – kama ilivyoelezwa katika 1 Joh 3:23-24: Hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri.Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

Soma Biblia Kila Siku 07/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More