Soma Biblia Kila Siku 07/2020Sample

Wala yeye hakumjibu neno (m.23). Huenda hata wewe uliwahi kuona hivyo ulipomwomba Yesu akusaidie katika jambo fulani. Huenda hata wewe unauguliwa na mtoto. Lakini Yesu amenyamaza tu. Ni kama hasikii. Hupati nafuu. Neno la leo, basi likusaidie. Kwanza utambue kwamba sisi wanadamu hatustahili lolote kwa Mungu, maana ni wenye dhambi na tunaishi katika ulimwengu wa dhambi. Hatuwezi kudai, ila kuomba tunaweza, tukiitegemea neema yake. Somo linatutia moyo tusichoke kuomba bali tudumu. Pia katika Mt 7:7-11 Yesu anatutia moyo vivyo hivyo, akiahidi, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? Au akiomba samaki, atampa nyoka?Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 07/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Related Plans

Recovering Hope: A 5-Day Devotional on the Intersection of Race, Mental Health, and Faith

Destined for the Cross

Overcoming Fear

Holy Week

Pray Like the Bible

30 Powerful Prayers for Your Child Every Day This School Year

Awakening Faith: Hope From the Global Church

You Say You Believe, but Do You Obey?

Rebuilt Faith
