YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 07/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

DAY 2 OF 31

Sura ya 13 ina mifano saba ya Yesu. Mifano hii inawasaidia wanafunzi wa Yesu kuelewa vizuri zaidi siri za Ufalme wa Mungu. Lakini kwao ambao hawajamkubali Yesu mifano haieleweki. Wasipoipokea kwa imani hawawezi kuielewa. Wenye mioyo migumu na mizito wanazidi kuwa wagumu wanapolisikia neno la Yesu. Ndugu msomaji, ukiwa na hali ya kutaka kulijua na kulielewa neno la Yesu, ni dalili kwamba moyo wako haujawa mgumu. Uzidi kumwomba Yesu akufunulie, naye hakika atakufunulia kwa nguvu ya Roho Mtaktatifu!

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

Soma Biblia Kila Siku 07/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More