Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mbazi za YesuMfano

The Parables of Jesus

SIKU 34 YA 36

WAKULIMA WAOVU
Kama mbazi nyinginezo, hii inahusu jibu letu. Tutaitikia kufanya jinsi Mungu anavyotaka? Ama tunakataa watu ambao Mungu ametuma na kuchagua nia zetu na ajenda zetu? Tunaishi maisha ya kutia juhudi ili "kuzaa matunda" kama ishara ya shukrani kwa Mungu kwani ametubariki kwa kutuwezesha kumtumikia? Mbazi hii inatukumbusha kuwa ni baraka kuu kuwa na uhusiano was kiagano na Mungu, lakini baraka hii ina majukumu.

Ni muhimu tujiuliza jinsi tunavyojibu waliotumwa na Mungu maishani mwetu. Mungu anaweza kuzungumza nasi kupitia malaika, ndoto, ama maono, lakini katika historia, amekuwa akizungumza na watu kupitia watu wengine. Watu wa Mungu walikataa manabii na kuchagua matakwa yao na kuelewa kwao, nasi pia tunaweza kukataa watu walio karibu nasi wanaotuambia ukweli wa Mungu kwa sababu kama zile za Wayahudi. Marafiki, familia, wanachama wa kanisa, na viongozi wa kanisa hawajaitwa kuhimiza kila tabia tunayofikiri ni njema. La, ikiwa wanapenda Yesu na wanatupenda kwa kweli, watakabiliana nasi na kuturekebisha ili tufanane na Yesu.

Una itikia vipi Mungu anapojaribu kukuhimiza au kukurekebisha kupitia watu wengine, Roho Mtakatifu, ama neno lake? Wewe ni mnyenyekevu na msikivu, ukitafakari kuhusu uliyoambiwa? Ama una kichwa ngumu, huwezi kubadilisha mienendo yako?

Kuhusu Mpango huu

The Parables of Jesus

Mpango huu utakuwezesha kusoma mbazi za Yesu na kuchunguza maana ya mafunzo yake kwako! Unaweza kuendelea na mpango wako ulipoachia kwani imerahisishwa kufika ulipokuwa. Hii itakupa wakati kutafakari na kuhamasishwa na upendo na nguvu wa Yesu!

More

We would like to thank Trinity New Life Church for this plan. For more information, please visit: http://www.trinitynewlife.com/