Furaha! kwa Ulimwengu Wako! Kujiandaa Kwa Krismasi

Ibada
Ni Krismasi!

Hembu twende safari ya Bethlehemu kwa kuangalia kwa makini hadithi ya Krismasi inayopatikana katika Biblia. Hadithi hii ya kihistoria ya kuzaliwa kwa Yesu haikuanzia Bethlehemu au hata Nazareti ... lakini ilianza na wanandoa wazee ambao walijua utimizo wa maisha mazuri waliyoishi kwa ajili ya Mungu.Biblia inawaelezea Elizabeti na Zakaria kwa njia moja ya kipekee ya upendo: "Walikuwa wenye haki machoni mwa Mungu, wenye kutembea kwa kufwata amri zote na matakwa ya Bwana." - luka 1:6

Elisabeti na Zakaria walikuwa wameoana kwa miaka mingi na bado walikuwa hawajajaliwa watoto. Maumivu ya moyo lazima yalikuwa machungu sana kwa huyu padri na mkewe, lakini Biblia inasema walizidi kutembea kwa uwepo wa Bwana na uhusiano wao na Bwana ulinawiri.

Je, huwa unajibu vipi masikitiko yakikukumba? Huwa unayatumia kama kisingizio cha kutenda kupita kiasi usiyostahili kufanya au huwa unalalamika na kunung'unika. Ingawaje Elisabeti na Zakaria walikuwa maskini bila matumaini, waliendelea kumtumikia Mungu kwa nyoyo zao zote miaka nayo ikiyoyoma tu.Biblia inasema kuwa maombi ya mwenye haki huleta mengi! (Yakobo 5:16) Unapoendelea kuishi maisha ya haki ... na kuendelea kuomba... maombi yako yatajibiwa.

Biblia inasema pia wenye haki huishi kwa imani. (Waebrania 10:38) Elisabeti na Zakaria waliendelea kutembea kwa imani na wala sio kwa kuona.

Jina la Elisabeti linamaanisha "Mungu ni Kiapo changu". Elisabeti aliamini katika ahadi za Mungu wakati wengine wangekuwa washa kata tamaa. Aliamini kuwa Mungu alikuwa anasikiliza maombi yake wakati marafiki wake waliwaimbia watoto wao na kisha baada ya miaka kuwabembeleza wajukuu wao kulala.

Natumaini kuwa somo la kwanza utajifunza katika hadithi ya Krismasi ni kuwa na subira na Mungu. Muamini Mungu hata kama mambo yako yamejaa na changamoto. Endelea kusihi maisha ya haki katika siku za masikitiko. Omba kwa bidii na amini kuwa Mungu anasikiliza maombi yako. Endelea kuwa na moyo wenye matumaini wakati njia zako haziendi sambamba na matumaini yako.Ruhusu upendo wa Elisabeti ukukumbushe kuwa waumini wa kweli hutembea kwa imani na wala sio kwa kuona.