Maelezo ya mpango
Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano
Ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana (m.8b). Yesu alikuwa ameonyesha mamlaka yake juu ya uumbaji. Kwa mwujiza huu Petro alikutana na utukufu wa Mungu. Ndipo akatambua sana upotevu wake! Maana kwanza alikuwa amejaa mashaka. Walikuwa wazoefu wa baharini. Kwenda kuvua samaki mchana wakati walikuwa hawajapata cho chote usiku ilikuwa haina maana kabisa. Hata hivyo akatii. Baada ya Petro kujitambua upotevu wake Yesu alimjibu nini? Tafakari ilivyoandikwa katika m.10: Usiogope, tangu sasa utakuwa ukivua watu. Je, wewe umetambua kuwa usipopata msamaha utapotea?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma k...
More
http://www.somabiblia.or.tz