Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

SIKU 18 YA 31

Mkazo wa Yesu ni huu: Umoja wa Wakristo ni wenye nguvu na muhimu kuliko umoja wa kiukoo. Ndiyo maana anaposema, Mama yangu na ndugu zangu ndio hao walisikiao neno la Mungu na kulifanya (m.19-21). Maana yake ni hii: 1. Hata kifo hakiwezi kuwatenganisha wanaomwamini Yesu. Wataingia wote katika uzima wa milele na kuwa pamoja daima. Bali umoja wa kiukoo huvunjika wakati wa kifo, maana wasiompokea Yesu huenda Jehanum. Kumbuka ahadi ya Bwana Yesu kwa wanafunzi wake: Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo (Yn 14:1-3). 2. Kwa suala la imani ni muhimu zaidi kumtii Yesu kuliko wazazi au ndugu. Mwenyewe anasema, Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili. Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona (Mt 10:37-39). Ila tusisahau kwamba Yesu aliwaheshimu wazazi wake! Ndiyo maana akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii (Lk 2:51; Yn 19:26-27).

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

http://www.somabiblia.or.tz