Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

SIKU 14 YA 31

Hakuna mtu aliyekuwa amemwomba Yesu amsaidie huyu mjane, maana hakuna mtu aliyetegemea kwamba Yesu ataweza kufanya mwujiza kama huu. Ni mara ya kwanza kwa Yesu kumfufua mfu. Alifanya hivyo kwa sababu alimwonea huruma huyo mjane ambaye maisha yake sasa yangekuwa magumu mno (m.13, Bwana alipomwona alimwonea huruma, akamwambia, Usilie). Badala ya kulia naye akasema Usilie. Badala ya kukaa mbali akakaribia na kuligusa geneza, tendo ambalo lilimnajisi kutokana na sheria za Wayahudi. Akasema neno tu akawa hai! Hofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu (m.16). Ukitaka kumtukuza Mungu vilevile, unaweza kutumia maneno ya Efe 3:20-21: Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina.

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma k...

More

http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha