Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

SIKU 8 YA 31

Yesu alipotabiri juu ya kubomolewa kwa hekalu, wanafunzi walidhani kuwa tukio hili linaendana na habari ya kurudi kwake kwa mara ya pili. Walipenda kujua ni matukio gani yatakayotangulia. Lakini hekalu lilibomolewa mwaka 70 BK, na matukio anayoyasema Yesu ni ishara au dalili juu ya kurudi kwake, ni kipindi kitakachoambatana na upinzani na mateso kwa waamini wake Yesu. Hata hivyo ushindi utakuwepo kwa watu wa Mungu watakaovumilia hata mwisho. Je, wewe umejiandaaje juu ya wakati huo?

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz