Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

SIKU 13 YA 31

Mji wa Yerusalemu ulitekwa mwaka 586 k.K. Usiku kabla habari hiyo haijafikia Babeli alipokuwepo Ezekieli, neno la Mungu tulilolisoma lilimfikia. Ezekieli alipotabiri juu ya Yerusalemu, ujumbe huo haukupokelewa. Sasa taarifa ya kutimia kwa unabii wa Ezekieli inapowafikia Waisraeli wanaoishi huko Babeli, wanaanza kuhimizana kufika kwa Ezekieli ili kumsikiliza. Wanafika kwa wingi – lakini hawayatendi (m.31, 32) maneno anayowapa Nabii. Tuwe wasikiaji na watendaji wa Neno, tukikumbuka Yesu analosema katika Yn 8:31-32, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz