Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano

Walioishi uhamishoni huko Babeli wanaonyesha dalili ya masikitiko kuhusu dhambi zao zilizopita. Baadhi yao wanataka kukata tamaa na kumlaumu Mungu kuwa hawatendei haki. Nabii anawakumbusha kwamba Mungu hapendelei kuadhibu tu, bali anataka watu wangetubu dhambi zao. Mungu yupo tayari kusamehe. Nabii anakaza zaidi kwamba kila mtu binafsi ana wajibu wa kutubu na kufanya yaliyo sawa. Maana kutambua makosa bila kuchukua hatua ya kuwajibikia na kutubu, hakumfanyi mtu kuwa mwenye haki.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz