Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

SIKU 31 YA 31

Tulijifunza katika somo la jana kwamba Daudi alitambua kuwa kimbilio liko kwa Bwana Mungu tu. Baada ya kutambua haya Daudi aliendelea kumsifu Mungu kwa utukufu wa kazi yake kwa wanadamu. Kwa ujumla Zaburi ya 40 ni zaburi ya sifa na utukufu kwa Bwana kwa yale aliyotutendea. Ieleweke kwamba, anayemsifu Mungu si lazima aelezee raha anayoipata tu. Bali katika sifa zake anayo hata nafasi ya kumwambia Mungu yale yanayomkosesha amani: Mabaya yasiyohesabika yamenizunguka mimi. Maovu yangu yamenipata, wala siwezi kuona. Yamezidi kuliko nywele za kichwa changu, na moyo wangu umeniacha (m.12). Kwa hiyo anaomba:  Ee Bwana, uwe radhi kuniokoa, Ee Bwana, unisaidie hima (m.13). Tuendelee kumsifu Mungu kwa kazi yake kwetu.

siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu k...

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha