Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano

Uongozi wake Mungu ni tofauti sana na ule wa wachungaji waovu: Mimi mwenyewe nitaamua kati ya kondoo wanono na kondoo wadhaifu (m.20 BHN). “Wanono” ni hao viongozi ambao kwa uchoyo na ubinafsi waliharibu malisho na maji ya kunywa. Wataachishwa kazi yao. Mungu atawaokoa “wadhaifu” vinywani mwa hao, akimweka “Daudi”, yaani, Masihi ili atawale watu wake. Masihi wa Bwana ni Mchungaji mwema. Baraka za uongozi wake ni pamoja na kuvunjika kwa nira ya utumwa na kuishi kwa usalama.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz