Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

SIKU 7 YA 31

Mgawo wa zawadi ya Mungu ni kinyume na wanadamu. Hakuna maendeleo na mafanikio yanayomzidi Kristo. Wokovu wa Mungu unawafikia wote sawa. Matajiri, maskini, wanyonge, wenye ulemavu, watoto kwa wazee, wote wana haki sawa katika wokovu. Hakuna anayebaguliwa wala kupokea wokovu kumzidi mwingine. Kinachotuzuia tusiupokee ni hiki tu kujiona kuwa wenye kitu (m.26, Angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa). Wito wetu ni kufungua mikono ya mioyo ili kumpokea Kristo kwa imani na kuendelea kuishi atuongozavyo. Soma tena m.30-31,Kwa [Mungu] ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kuji...

More

Tungependa kushukuru kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha