Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kazi ya injili katika janga la COVID-19Mfano

Gospel Driven Work In The COVID-19 Crisis

SIKU 4 YA 4

Sina uhakika juu yako, lakini mpaka hivi karibuni, siku zote nilisikia Wafilipi 6 na 8 kama tofauti, maagizo yasiyohusiana. Lakini kama tuonavyo katika maandiko ya leo, sura hizo zina shabihiana, zikitenganishwa na sura ya 7 tuu. Je hiyo yawezekana ni kwa sababu sehemu ya majibu ya wasiwasi yetu iko juu ya kile tunachochagua kukifikiria?

Kwa akili ya kawaida tuu na uzoefu wetu wa kufanya kazi wakati wa janga la COVID-19, nafikiria jibu kwa swali hilo ni " ndiyo". Paulo anatuamuru kutawala mawazo yetu Ili Bwana atuweke huru na wasiwasi.

Nyakati hizi zinatoa ushuhuda wa kweli hii.

Habari za leo si nzuri au za kupendeza. Mbali na hapo. Vichwa vya habari leo vimejaa hofu na wasiwasi.

Ni kweli tunahitaji kuhabarishwa juu ya mambo yanayoendelea katika jamii tunayoishi na katika sehemu za kazi. Lakini hiloHali Maanishi kuwa tunahitaji kusoma, kuangalia, au kusikiliza habari kwa muda wote mpaka mwisho.

Ukisikiliza podcast yangu, Wito wa kuwa mahili, yawezekana umenisikia nazungumzia ukweli kwamba ninapokea taarifa Taarifa Sufuri: Hakuna cnn.com, hakuna Twitter, hakuna magazeti, hakuna MSNBC or Hakuna habari za FOX. Hakuna.

Lakini kwa sababu zilizo wazi, hivi karibuni nimeanza kuangalia Wavuti za habari kuhusu maelekezo ya kujitenga, kufungwa kwa shule, nk. Taarifa hizi zilikuwa ni muhimu sana kwa maisha yangu na kazi.

Lakini katika kutafuta taarifa hizo muhimu, nilikutana na chombo cha habari za kisasa, wakinukuu vichwa vya habari kutoka (“Hulk Hogan: ‘labda hatuhitaji chanjo’”) na taarifa za hofu (“idadi ya vifo Marekani yakaribia 10,000”). Ni wazi, habari hii ( ikiwa inaburudisha na kutaarifu) haiathiri maisha yangu au kazi yangu hata kidogo.

Siku chache baada ya kurudi kwenye kusikiliza habari, nilianza kuwa na kiwango fulani cha wasiwasi ambachoSijawahi Kuhisi huko nyuma. Baada ya kutafakari juu ya mstari huo, mhusika alikuwa dhahiri kwangu. Badala ya kujaza akili yangu kwa neno la Mungu na kujikumbusha ahadi zake, nilikuwa najaza akili yangu na visivyofaa, na habari za kutia wasiwasi.

Wewe na mimi tunaweza kuwa tunaangaliwa na wafanyakazi wenzetu kutafuta tumaini katika nyakazi hizi za kujaribiwa. Lakini haitakuwa hivyo ikiwa sisi wenyewe tumekuwa Na wasiwasi na wasahaulifu wa tumaini tulilonalo katika Kristo. Hebu na tue ni watu wa kujaza mawazo yetu ambavyo ni " kweli, adili, sahihi, safi, vya kupendeza, bora [and] vyenye sifa” ili kwamba tumaini la injili ling'ae kwa tunaofanya nao kazi na kuishi nao.

Kama umefurahia mpango huu, utafurahia ibada yangu wa juma, ikikusaidia zaidi kuunganisha injili na sehemu yako ya kazi. Jiandikishehere.

Kuhusu Mpango huu

Gospel Driven Work In The COVID-19 Crisis

Unafanyia kazi nyumbani? Umejitenga na jamii? Katika mpango huu wa siku nne, utasoma kitabu chote cha Wafilipi ( ambacho Paulo alikiandika akiwa gerezani) kupata mtazamo wa kibiblia, tumaini na miongozo ya namna tunavyoweza kufanya kazi katika kipindi hiki cha janga la COVI-19.

More

Tungependa kumshukuru Jordan Raynpr kwa kutupa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea https://jordanraynor.com/covid19/