Kazi ya injili katika janga la COVID-19Mfano

Jana, tuliangalia Wafilipi 1 na jinsi Paulo alivyotumia muda wake wa kutengwa " kupeleka mbele injili." Moja ya njia tunazoweza kutumia muda wetu wa kutengwa ni kwa kufuata maagizonya Paulo katika maandiko ya leo “kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake, Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine (Wafilipi 2:3-4).
Ni rahisi kutoa huduma ya maneno tuu kwenye hili wakati ulimwengu una afya ya kutosha kimwili na kiuchumi. Na ni kitu kingine kabisa kuacha kuelezea injili katika nyakati kama tulizo nazo sasa.
Twawezaje kuwathamini wengine kwa matendo kuliko sisi wenyewe nyakati hizi? Jibu la swali hilo litakuwa tofauti kwa kila mmoja wetu kulingana na majukumu yetu na hali zetu za kifedha. Lakini hapa kuna mapendekezo machache.
Kaa nyumbani. Wengi wetu tuko chini ya maagizo na matangazo kutoka mamlaka za erikali ya kujitenga na wengine. "Wathamini wengine kuliko mwenyewe" wa kufuata maelekezo haya, kujitolea uhuru wako binafsi kwa ajili ya kuwajali majirani zako.
Wanaojitolea wanapata mshahara pungufu ili kulinda kazi za wengine.Watu wachache wanaweza kufanya hivi, lakini wanaofanya hivyo wana fursa ya kuhubiri injili kupitia matendo.
Toa kwa moyo mkunjufu kuliko ulivyokuwa. Juma lililopita, nilizungumza na rafiki anayeendesha wakala wa matangazo ya kidigitali. Wakati biashara yake haijaathirika sana na janga hili, ana kila sababu kuamini itaathirika. Lakini baada ya maombi mengi, aliamua kuchukua hatua ya imani kulipia pango mgahawa wake ambao ulikuwa unaelekea kufilisika. Matendo kama haya yanaweza kuonekana yakipuuzi, lakini kwa wenye migahawa, inaonekana kama ni injili katika matendo.
Nachopendekeza hapa ni hard. Lakini unajua kitu ambacho ni kigumu kukielewa vizuri? Kulipa kwa ajili ya dhambi zetu. Tumeitwa kuonesha maisha ya kujitoa mfano wa maisha ya Yesu. Basi nasi tuone ni kwa jinsi gani tunaweza kufanya kazi ya injili katika kipindi hiki cha janga hili.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Unafanyia kazi nyumbani? Umejitenga na jamii? Katika mpango huu wa siku nne, utasoma kitabu chote cha Wafilipi ( ambacho Paulo alikiandika akiwa gerezani) kupata mtazamo wa kibiblia, tumaini na miongozo ya namna tunavyoweza kufanya kazi katika kipindi hiki cha janga la COVI-19.
More