Kazi ya injili katika janga la COVID-19Mfano

Kijitenga kwa njia ya kifungo haikuwa katika mpango wa Paulo.
Ukitazama, kigungo chake kinaweza kuwa kilionekana kama ni kuvuruga majaribio yake ya kutangaza injili kupitia kazi zake kama mtengeneza mahema na mhubiri. Lakini Paulo alisema waziwazi kwamba " kilichotokea kwangu kimenisaidia kuendeleza injili" ( Wafilipi 1: 12).
Kwa vipi? Kama Wafilipi 1:13 inavyoweka wazi, injili iliweza kung'aa sana kwa sababu ilimpa Paulo nafasi ya kuonesha kwamba, pasipo kujali mazingira, hatimaye alikuwa "kifungoni kwa sababu ya Kristo," Kwa hiari akifungiwa kwenye uhuru wa Mungu.
Tumaini hilo katika muktadha wa mazingira ya Paulo yaweza kuwa ilionekana katika ulimwengu "ulinzi wote wa ikulu." Hivyo, hata wao walikuja kuelewa tumaini la injili.
Tunaweza kujifunza nini katika maandiko haya wakati wewe na mimi tunafanya Kazi na kuishi katika mazingira ya kutengwa? Sisi, kama Paulo, tuna nafasi za pekee Kuonesha tumaini la injili, siyo Pasipo kujaliMazingira yetu, lakini kwa sababu yao. Kwa jinsi gani?
Kwa kuwaonesha tunajali, lakini hatuna wasiwasi. Je, tuna sababu ya kujali kuhusu virusi vya korona? Dhahiri. Je tuna sababu ya kuwa na wasiwasi? Ni wazi hapana, kwa sababu tuna "Amani ya Mungu, ipitayo fahamu zote" kwa sababu ya Kristo na ahadi yake ya kutukomboa na ulimwengu ( Wafilipi 4:7). Katika wakati huu wa usalama kuwa mdogo, usalama wetu unaweza kuwavuta wengine kama wafanyakazi wenzetu, wateja, na marafiki.
Kwa kuonesha kuwajali kwa tofauti wote wanaotuzunguka. Zaidi ya ilivyowahi kutokea, wafuasi wa Kristo wanatakiwa kuwa ndiyo wanaoonesha kuwajali huko watu tunaofanya kazi nao, zaidi ya "thamani" wanayotoa kwenye kampuni na makundi yetu. Huu ni wakati ambao kuuliza maswali mengi binafsi kuhusu siyo tu yanakubalika, lakini yanaonesha utu. Hebu tuwe wafanyakazi wenza wanaojulikana kwa kujadi sana kwa watu tunaofanya nao kazi kila siku.
Kwa kushirikiana tumaini letu waziwazi Mapendekezo mawili yanaweza kutumika kama vidokezo kwenye injili kama motisha yetu ya upendo kwa majirani, lakini wakati mwingine, lazima tushirikiane nao injili kwa maneno. Sasa ni wakati bora zaidi. Watu katika ofisi zetu na majirani wanatafuta tumaini zaidi. Tumaini la kazi yao. Tumaini leo wenyewe. Kama wakristo, tuna chanjo ya kiroho ambayo inaweza kuleta tumaini milele. Hebu tuwe wajasiri sana kushirikiana na "kutangaza injili pasipo hofu" (Wafilipi 1:14)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Unafanyia kazi nyumbani? Umejitenga na jamii? Katika mpango huu wa siku nne, utasoma kitabu chote cha Wafilipi ( ambacho Paulo alikiandika akiwa gerezani) kupata mtazamo wa kibiblia, tumaini na miongozo ya namna tunavyoweza kufanya kazi katika kipindi hiki cha janga la COVI-19.
More