Kazi ya injili katika janga la COVID-19Mfano

“Kila kitu [is] Chini ya mamlaka yake” (Wafilipi 3:21). Ni ukweli wa utukufu kiasi gani kuushikilia leo.
Mungu anatawala afya zetu.
Anatawala uchumi wetu.
Anatawala kazi zetu.
Na japo tunaweza tusielewe au kufahamu mipango yake, kupitia maandiko, amethibitisha kuwa mwaminifu na huru, akifanya vitu vyote kwa utukufu na mwishowe " mema kwa wote wampendao" ( Warumi 8:28).
Siku moja, tutaona kilele cha wema huo katika ulimwengu mpya ambapo Kristo atatawala kama mfalme milele. Lakini mpaka wakati huo, mfalme ametuita kufanya kazi kama mawakili wake, tukijibidiisha kuongeza utawala wake na ajenda yake ya ukombozi kila eneo la uumbaji wake.
Madaktari wanafanya kazi masaa 24 kuidhibiti COVID-19.
Viongozi wa serikali wanajitahidi kuthibiti mtindo wa maisha yetu.
Wajasiriamali nao wanajitahidi kuweka uchumi katika njia sahihi.
Kazi zetu zote zinatakiwa kulenga katika kurejesha kilichoharibika katika ulimwengu wetu leo, kulingana na ajenda ya mfalme mmoja wa kweli. Lakini ikiwa tutafanikiwa ama tutashindwa, juhudi zetu zote katika kazi ya ukombozi zina nafasi ya kutumika kama ishara katika ukombozi kamili kupitia Kristo.
Katika asubuhi ile ya pasaka, Yesu alituonesha kwamba ana nguvu " za kubadilisha miili yetu" kwa kukombolewa, kuwa kamili, na " yenye utukufu" (Wafilipi 3: 21). Lakini kama maandiko yanavyoweka wazi, Yesu atakaporudi kutawala milele katika Yerusalemu mpya, hatakomboa miili yetu tuu. Atakomboa Uumbaji wote. Kwa sababuKila kituMwishowe kiko chiniYa Utawala wake.
Siku moja, jitihada zetu zote za kazi ya ukombozi zitakamilika. Mpaka siku hiyo, tufanye kazi kwa moyo wote (Wakolosai 3:23) tukielekeza tumaini lijalo kwa ulimwengu wetu.
Kuhusu Mpango huu

Unafanyia kazi nyumbani? Umejitenga na jamii? Katika mpango huu wa siku nne, utasoma kitabu chote cha Wafilipi ( ambacho Paulo alikiandika akiwa gerezani) kupata mtazamo wa kibiblia, tumaini na miongozo ya namna tunavyoweza kufanya kazi katika kipindi hiki cha janga la COVI-19.
More