Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kusikia kutoka Mbinguni: kusikiza Mungu kila siku.Mfano

Kusikia kutoka Mbinguni: kusikiza Mungu kila siku.

SIKU 5 YA 5

Sauti Ya Mbinguni Yasema ‘Jifiche Ndani Yangu’


Nikikua, nilkuwa kijana mdogo. Na bado mimi ni mdogo.


Maisha katika mabanda ya nairobi huwa yana sifa za vurugu-na kukosa uhakika kwangu, kulinipa sehemu yangu ya hiyo vurugu. Mara zingine, nilihisi maisha ni kama kila anashughulika na shida zake. Wazazi wetu hawakuwa na wakati wa kutulinda kutokana na kuonewa- kwani ilibidi wafanye kazi vile wangeweza hili wapate mapato.


Nikiwa darasa la sita, nilipitia katika hali ya kuonewa shuleni na wanafunzi wengine. Kiongozi wao alikuwa kama jitu, na alinifedhehesha sana. Mwisho wa wiki, nilijipata nakata tamaa. Lakini nilienda kwa kituo cha compassion kanisani kwetu, ambapo walifundisha kuwa mungu ni kimbilio letu. Nilipokuwa nikisikiza mafundisho haya, upendo wa bwana ulinijaa na roho yangu ikafarijika.


Katika kituo hicho cha compassion, ndipo mahali niliweza kuhisi amani na usalama. Wafanyikazi wa compassion, walitulinda na kutupa faraja.


Hushawahi kuwa na hofu? Hushawahi hisi hauko salama? Hushawahi jihisi kuwa hauwezi kuhifadhi maisha yako? Tunaweza mpelekea mungu hofu yetu, maana yeye ni mungu mwema. Yeye usikia vilio vyetu vya usalama. Na utulinda kutokana na maovu. 


Kama Daudi, unaweza kumuita mungu. Anaweza kuhifadhi maisha yako! Anaweza kukulinda kutokana na hatari za dunia. Chukua muda na uombee watoto wote duniani ambao wana hofu kuhusu maisha yao. Omba kwa ajili ya maisha na nafsi zao, hili mungu aweze kujionyesha kwao kama kimbilio lao. Amina.


Soma zaidi kuhusu mpango wa compassion, ambao mwandishi wetu Njenga anaongelea kuhusu, na vile unavyoweza kusaidia kuleta roho wa mungu katika maisha ya watoto walio katika umaskini, kupitia tofuti ya help bring the Spirit of the Lord to children in poverty.

siku 4

Kuhusu Mpango huu

Kusikia kutoka Mbinguni: kusikiza Mungu kila siku.

Bwana yu hai na ni mkamilifu leo, na uongea na kila mtoto wake moja kwa moja. Lakini wakati mwingine, inaweza kuwa ngumu kumuona na kumsikia Mungu. Kupitia kuchunguza hadithi ya safari ya mtu mmoja ya kufahamu sauti ya M...

More

Tunapenda kushukuru Huruma ya Kimataifa kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.compassion.com/youversion

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha