Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kusikia kutoka Mbinguni: kusikiza Mungu kila siku.Mfano

Kusikia kutoka Mbinguni: kusikiza Mungu kila siku.

SIKU 1 YA 5

Ukweli Kutoka Kwa Roho


Baada ya kufikisha miaka kumi na tano ya kuzaliwa, niliacha kwenda kanisani. Nilitaka kufurahia maisha, na kanisani hapakuwa mahali pazuri pa kufurahia. Niliishi maisha ya uasi na nilijipata kwa shida nyingi sana. Nikikumbuka maisha ya ujana wangu, yananikumbusha vile ukweli wa Mungu ulibainika kwangu. Mungu alitumia ukweli wake kunitoa gizani.


Roho mtakatifu uongea na kuonyesha ukweli kwa wanaoamini na wasioamini. Katika ujana wangu wa uasi, roho wa Mungu alijithirihisha kwangu. Hapo ndipo nilipotambua ya kwamba nilikuwa katika njia ya giza na mauti. Nilihitaji mwangaza wa mungu na uhai. Ilibidi nisimamishwe kutoka shule kwa muda wa wiki mbili, ili Mungu aweze kujithihirisha katika maisha yangu. Katika muda huo wa wiki mbili nje ya shule, roho mtakatifu alinizungumzia na kuniongoza kuziacha njia zangu mbaya.


Kama waumini, hatuko peke yetu. Roho mtakatifu uongoza matendo yetu na pia yeye usema nasi. Tunahitaji ukweli wa Mungu kila siku, ambao Roho Mtakatifu utupa. Lakini wakati mwingine hatusikizi na kwa hivyo hatusikii. Tunadhani kwamba Mungu hazungumzi. Lakini hivyo ni kweli? Inawezekana kwamba hatujajua jinsi ya kumsikiliza Mungu. Roho mtakatifu unena maandiko ya Biblia katika maisha yetu.


Haiwezakani kwa mwenye dhambi kukubali ukweli bila roho mtakatifu kumthihirishia ukweli. Pia haiwezekani kuishi maisha matakatifu kama roho wa kweli hajathihirishia mtu njia ya haki.


Kila muumini upewa roho mtakatifu, ili amfungue macho na kumuonyesha mpango wa mungu. Naomba tuchukue muda kidogo na tuombe hili roho mtakatifu aweze kuwafungua macho wale ambao wamepofushwa na giza la shetani. Baba wetu aliye mbinguni,asante kwa roho anaye nena nasi na kutuonyesha ukweli. Naomba kuwa utanena na kuonyesha ukweli wako kwa wengi wanaotembea katika maisha ya giza, Amina!

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Kusikia kutoka Mbinguni: kusikiza Mungu kila siku.

Bwana yu hai na ni mkamilifu leo, na uongea na kila mtoto wake moja kwa moja. Lakini wakati mwingine, inaweza kuwa ngumu kumuona na kumsikia Mungu. Kupitia kuchunguza hadithi ya safari ya mtu mmoja ya kufahamu sauti ya M...

More

Tunapenda kushukuru Huruma ya Kimataifa kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.compassion.com/youversion

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha