Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kusikia kutoka Mbinguni: kusikiza Mungu kila siku.Mfano

Kusikia kutoka Mbinguni: kusikiza Mungu kila siku.

SIKU 3 YA 5

“MIMI NIKO Amenituma Kwenu”


Nikiwa mtoto, nilipenda sana kusikiza hadithi za wana wa Israeli wakiokolewa na mungu kutoka misri. Nililinganisha maisha yangu na hizi hadithi. Kwani kuishi, maisha ya umaskini uliokithiri, ililingana sawa na kuishi kwa utumwa huko misri.


Ukiishi maisha yako katika mabanda ya Nairobi, Kenya itakulazimu umtafute mungu. Itakubidi umuombe mungu akuokoe kutoka kwa umaskini ambao jamii yako inaonekana haiwezi kuepuka. Nilipojua kuwa mungu anaweza kusikia kilio changu, ilinipa faraja moyoni, kwamba atanisaidia. Kama mwandishi wa zaburi, niliweza kulia, “je usaidizi wangu watoka wapi? Usaidizi wangu watoka kwa bwana, muumba wa mbingu na nchi.”


Hadithi ya kutoka ilionyesha wazi kuwa mungu usikia kilio cha watu wake. Alisikia kilio cha mara kwa mara kutoka kwa watu wake, na akataka kuwaokoa kwa ajili ya ufalme wake. Na anakuona pia wewe. 


Zaidi ya yote, mungu alimchagua kiongozi wa kuongoza watu wake kutoka kwa utumwa. Mungu alimuakikishia musa kwamba atakuwa pamoja naye- “MIMI NIKO amenituma kwenu.” Musa alihitaji kusikia na kujua ni nani alikuwa akimuita. Kama waumini, tunahitaji kukumbuka ni nani alituita kwa maisha tunayoyaishi. Yesu, MIMI NIKO, ako pamoja nasi. Ni yeye anayetuongoza, na kutuwezesha kukamilisha kazi ambayo ametuita tufanye.


Bwana aliwaona wana wa Israeli wakiteseka misri, na akawaokoa.


Je unamsubiri Mungu? Je umehisi kama itachukua milele? Tunamngojea mungu kwa uvumilivu, tukiwa katika hali ya umaskini, ugonjwa, utajiri, na hali zingine zote, kwa sababu tunajua yeye usikia maombi yetu na kuona hali zetu.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Kusikia kutoka Mbinguni: kusikiza Mungu kila siku.

Bwana yu hai na ni mkamilifu leo, na uongea na kila mtoto wake moja kwa moja. Lakini wakati mwingine, inaweza kuwa ngumu kumuona na kumsikia Mungu. Kupitia kuchunguza hadithi ya safari ya mtu mmoja ya kufahamu sauti ya M...

More

Tunapenda kushukuru Huruma ya Kimataifa kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.compassion.com/youversion

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha