Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kusikia kutoka Mbinguni: kusikiza Mungu kila siku.Mfano

Kusikia kutoka Mbinguni: kusikiza Mungu kila siku.

SIKU 4 YA 5

Baba Wako Wa Mbinguni Anajua Mahitaji Yako Yote


Kukulia Nairobi ilikuwa ni maisha magumu sana. Miaka ya 1990’s ilikuwa ni misukosuko ya maisha. Maandamano yalikuwa ni hali ya kawaida, ilisababishwa na pinzani kati ya chama tawala na wale waliokuwa wakipigania mfumo wa vyama vingi. Wakati wa maandamano, maskini ndio uteseka sana. Maskini utegemea mapato yao madogo ya kila siku, ili kutimiza mahitaji yao ya kila siku, kwa hivyo hizi pinzani ziliwafanya maskini kuteseka zaidi.


Kutokana na hali hii, maisha yalinifunza kuwa na subira kutoka nikiwa mdogo wa miaka.


Wakati hakuna uhakika wa matokeo mazuri, kusubiri kunaweza kuwa kazi ngumu sana. Baba yangu alikuwa kibarua, kwa hivyo tulitegemea mapato yake ya kila siku kutimiza mahitaji yetu ya msingi. Alikuwa akipata kibarua, tukawa tutakula, lakini hakikosa tulikuwa hatuli.


Baba yangu alitusomea mathayo 6:25-34 siku moja wakati wa ibada yetu kama familia. Alisisitiza umuhimu wa kuweka tumaini letu ndani ya yesu. Haya maneno ya yesu yalinipa tumaini katikati ya kutokuwa na uhakika wa maisha kwetu. Kama familia, tulitulia ndani ya uhakika wa kwamba, baba wetu wa mbinguni alijua mahitaji yetu yote. Kumjua na kuwa na yesu ilitosha.


Baba yetu aliye mbinguni anajua yote tunayohitaji. Ni ajabu hipi hii? Kwamba mungu aliyeumba kila kitu,ni yeye bado anayetimiza mahitaji yetu.


Ni rahisi kutia shaka kwamba atatimiza ahadi zake. Ni nini kitafanyika kama hatatimiza mahitaji yangu ya fedha? Afya yangu? Jamii yangu? Na (jaza mahitaji yako)? Jifunze kuweka tumaini lako ndani ya bwana, hata kama hali yako ni ngumu vipi. Jitolee kusoma na kufuata neno la mungu kila siku, huku ukisubiri jibu kutoka kwa mungu.




Kupitia subira, tumaini letu linapata nguvu. Kama watoto wa mungu, tunamsubiri mungu mwaminifu na mwenye upendo, ambaye ufurahi wakati anatimiza mahitaji ya watoto wake. Muombe mwokozi wako: “Bwana wangu, kama mtoto wako, mimi ujipata na wasiswasi kuhusu maisha yangu ya usoni. Lakini leo, naeka tumaini langu kwako, kwa sababu wewe peke yake ndiwe uliye mwaminifu katika maisha yangu. Amina.”

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Kusikia kutoka Mbinguni: kusikiza Mungu kila siku.

Bwana yu hai na ni mkamilifu leo, na uongea na kila mtoto wake moja kwa moja. Lakini wakati mwingine, inaweza kuwa ngumu kumuona na kumsikia Mungu. Kupitia kuchunguza hadithi ya safari ya mtu mmoja ya kufahamu sauti ya M...

More

Tunapenda kushukuru Huruma ya Kimataifa kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.compassion.com/youversion

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha