SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20Mfano

Kwa mistari hii, Daudi anazidi kumsifu Mungu. Anamsifu kwa ajili ya wokovu wake na ukuu wake. Pia anaelezea furaha yake kubwa ya kuingia katika nyumba ya Mungu pamoja na watu wake. Kipekee tunapata katika zaburi hii unabii juu ya wokovu kwa baadhi ya Waafrika. Kushi (ambayo ni sawa na Ethiopia) itamnyoshea Mungu mikono yake mara (m.31). Kama ilivyoandikwa katika Mdo 8:27-38, mtu wa Kushi ndiye Mwafrika wa kwanza aliyesikia Injili (hata kabla ya watu wa Ulaya); na siku hizi kuna uamsho mkubwa sana Ethiopia, na mamilioni ya watu wamempokea Yesu Kristo nchini hapo na barani Afrika kwa ujumla!
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Kutoka, Zaburi na Isaya. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Anza mwaka wa 2020 kwa kujifunza Neno la Mungu kupitia mpango huu.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz
Mipangilio yanayo husiana

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Upendo Wa Bure

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?

Soma Biblia Kila Siku 11/2020

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021
