Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 1Mfano

Soma Biblia Kila Siku 1

SIKU 9 YA 31

Jambo muhimu sana ni kiu ya kutafuta kuuingia ufalme wa Mungu. Nikodemo alikuwa nayo. Na wewe, je? Kama unayo kiu hii, basi, sikiliza kwa makini maelezo ya Yesu mwenyewe akifunua siri ya namna ya kuuingia ufalme wa Mungu: Zaliwa mara ya pili! Fikiria mtoto anavyozaliwa. Si utashi na nguvu zake mwenyewe zinazofanya hiyo, bali ni kazi ya mzazi. Kwa hiyo kuzaliwa mara ya pili ni tendo la Mungu. Mungu anamzaa mara ya pili kila mtu anayemwamini Yesu Kristo na kubatizwa kwa maji na kwa Roho.

Andiko

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 1

Soma Biblia Kila Siku 1 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Injili ya Yohana, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha